Friday, February 15, 2013

Nyangumi

Nyangumi ni mamalia wa bahari, au pengine wa maji matamu, katika oda Cetacea wanaofanana na samaki. Kwa hivyo hawatagi mayai kama samaki lakini huzaa watoto kama mamalia wote na huwanyonyesha. Pamoja na nguva wanyama hawa ni mamalia wa pekee wanaoishi kwenye maji tu. Oda yao ina mnamo spishi 80. Spishi ndogo huitwa pomboo kwa kawaida na spishi kadhaa za pomboo huishi kwenye maji matamu ya mito mikubwa kama Ganges au Amazonas.
Mwili wote unalingana na maisha ya majini. Nyangumi wanaotupwa kwenye nchi kavu wanakufa haraka; wanakauka, uzito wa mwili unagandamiza mapavu kwa sababu wanakosa ueleaji wa maji.
Hata hivyo muundo wa mwili bado ni sawa kama mamalia wengine:
  • wanapumua kwa kutumia mapafu; kutegemeana na spishi zinaweza kuzama na kukaa chini ya maji kuanzia dakika kadhaa hadi masaa mawili.
  • Huwa na moyo yenye vyumba viwili inayoweza kusambaza oksijeni mwilini kote.
  • Nyangumi huwa na damu moto yaani wanaweza kutunza halijoto ya wastani mwilini tofauti na samaki wanaobadilika halijoto ya mwili kulingana na halijoto ya mazingira.
  • Wanazaa watoto waliokamilika tayari na kuwanyonyesha maziwa yenye mafuta mengi kwa kutumia viwele vyao. Kiinitete hukua mwilini hadi kuwa mnyama kamili jinsi ilivyo na mamalia wengi.
Spishi nyingi za nyangumi ni kubwa sana. Nyangumi buluu (Blue whale) anaweza kufikia uzito wa tani 200 na urefu wa mita 33. Nyangumi wadogo ni hasa familia ya pomboo ambao wadogo wanafikia urefu wa mita na nusu pekee.
Mara nyingi spishi za nyangumi zinatofautishwa kutokana na meno yao:
  • wale wanaovinda samaki au wanayama wakubwa wengine wa bahari wana meno ya kawaida.
  • wale wanaokula planktoni (viumbe vidogo sana baharini) hawana meno bali mifupa ya kinywani ambao si mifupa ya kweli inaundwa na kitu kinachofanana na kucha za vidole. Mifupa hii inakaa kama meno ya chanuo inafanya kazi ya filta; nyangumi huyi anafungua mdomo na kujaza nafasi maji pamoja na yote yaliyomo kama uduvi wadogo sana; ulimi unasukuma maji kupitia chanua ya mifupa ya kinywani na windo unabaki ndani kama chakula.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Eutheria
Oda ya juu: Laurasiatheria
Oda: Cetacea (Wanyama kama nyangumi)

0 comments:

Post a Comment